Ni stori kutokea katika kijiji cha Mtegu kilichopo Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara ambapo wananchi wamelalamika baada ya kuwepo sintofahamu ya kufunguliwa kwa Kituo cha Afya.
Kituo hicho kimejengwa kwa nguvu za wananchi tangu mwaka 2006 wakichangia nguvu kazi, vifaa vya ujenzi na pesa taslim kupitia makato ya shilingi 50 kwa kila kilo ya korosho ambayo wanauza wananchi hao.
Wananchi hao waliahidiwa kituo hicho kitafunguliwa mwezi September 2017 ahadi ambayo haijatekelezwa na hivyo wananchi kuendelea kufuata huduma za kitabibu katika kijiji cha Luagala umbali wa kilometa 35.
TAASISI YA MIFUPA MUHIMBILI (MOI) IMEFANIKISHA UPASUAJI WA KICHWA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA