Asubuhi ya leo January 6, 2017 Rais John Magufuli amemtembea Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombalemwiru aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mzee Kingunge anapatiwa matibabu ya majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam siku chache zilizopita.
Leo ni siku ya pili baada ya kifo cha mkewe Peras na hadi siku ya jana msemaji wa familia hiyo Tony Ngombalemiru alieleza kuwa bado walikuwa hawajampa taarifa hizo za msiba Mzee Kingunge kutokana na hali yake.
FAMILIA YA KINGUNGE: MZEE ALING’ATWA NA MBWA, TUNAANGALIA JINSI YA KUMUELEZA KUHUSU MSIBA