Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso, amesema Serikali haitavumilia wakandarasi wasio na uwezo (wakandarasi mbeleko) ambao wanapewa kazi lakini wanashindwa kuzimaliza kwa muda uliopangwa.
Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Shinyanga na wakazi wa kijiji cha Mendo, katika ziara yake ya siku 5 inayolenga kukagua maendeleo ya miradi ya maji mkoa wa Shinyanga, Aweso amezungumzia mwenendo wa utekelezaji usioridhisha wa mradi wa maji kijiji cha Mendo.
Aweso amekukagua mradi ulioanza kutekelezwa Aprili 2014 na ulitarajiwa kukamilika mwezi December 2017 lakini mpaka sasa haujakamilika, mradi ambao una gharama ya zaidi milioni 300 na unatarajiwa kukamilika mwezi huu January 2018.
“Nikuombe sana Mkurugenzi wa Halmashauri, hakikisha mnatafuta wakandarasi wenye uwezo, Miradi mingi ya serikali imekua ikifa, inakua siyo yenye tija kwasababu tunawapa wakandarasi Mbeleko” – Aweso
KOSA ALILOLIBAINI RC. MAKONDA KATIKA TUKIO LA MOTO BUGURUNI