Ni wachezaji wachache wa Afrika ambao wamewahi au wanapata nafasi ya kujiunga na Ligi Kuu England, hiyo inatokana na utaratibu wao ili usajiliwe katika club hizo kwanza timu yako ya taifa lazima iwe nafasi nzuri katika viwango vya FIFA au uwe ni mchezaji mwenye kipaji.
5. Nwankwo Kanu amewahi kucheza soka England kwa kipindi cha muongo mmoja akivichezea vilabu vya Arsenal F.C, West Bromwich Albion F.C na Portsmouth F.C lakini amedu Arsenal kwa miaka 6 na kufunga jumla ya magoli 54 EPL, Mataji mawili ya EPL na FA mawili.
4. Yaya Toure ni staa wa kimataifa wa Ivory Coast na club ya Man City ya England lakini bado anatajwa kuwa na nafasi ya kufunga magoli zaidi kutokana bado anacheza tofauti na Kanu ambaye ameshastaafu, Toure amefunga jumla ya magoli 59.
3. Yakubu Aiyegbeni ni staa wa soka wa kimataifa wa Nigeria ambaye amewahi kucheza England katika vilabu mbalimbali ikiwemo Everton lakini Yakubu amefunga jumla ya magoli 95 akiwa EPL na kwa sasa anaichezea Coventry City inayocheza Ligi daraja la pili England.
2. Emmanuel Adebayor kwa sasa anaendeleza maisha yake ya soka akiwa Uturuki katika club ya İstanbul Başakşehir lakini amewahi kuvichezea vilabu vya Arsenal, Man City, Tottenham na Crystal Palace vyote vya England, Adebayor yeye hadi anaondoka EPL amefunga jumla ya magoli 97.
1- Didier Drogba ameichezea Chelsea kwa muda mrefu lakini pia ni moja kati ya wachezaji wa kiafrika wenye heshima kubwa katika soka la England kutokana na uwezo wake aliowahi kuuonesha, Drogba amefunga jumla ya magoli 104 EPL na amestaafu soka akiwa na miaka 39.
Alichokifanya Simon Msuva kwa Wakati Ujao Youth Academy