Leo January 16, 2018 Mbunge Kigoma Mjini na Kiongozi wa chama cha ACT wazalendo Zitto Zuber Kabwe ameonesha kutokuridhishwa na uamuzi wa jeshi la polisi mkoani Kigoma baada ya kuzuia Mkutano wa hadhara wa Mbunge huyo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Zitto Kabwe ameandika “Jeshi la polisi limezuia Mkutano wangu wa hadhara kama Mbunge wa Kigoma Mjini kinyume na sheria ya Bunge ya mwaka 1988. Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inayolazimisha Mbunge kufanya mkutano kwenye jimbo lake bila vikwazo”.
“Sitaki kuwapa polisi sifa ya kupambana nasi. Tumeghairisha mkutano mpaka siku ya jumamosi, tumewaandikia barua rasmi kuwa sheria waliyoinukuu sio sheria halali na haihusiani na mikutano ya Mbunge kwenye jimbo lake. Sheria wanayopaswa kunukuu ni sheria namba 3 ya mwaka 1988 kifungu cha 4(1). “- Zitto Kabwe
“Ofisi yangu itamwandikia Spika wa Bunge rasmi kuhusu suala hili ili lisifanyike kwa Mbunge mwingine yeyote”. -Zitto Kabwe
VIDEO: WAFANYAKAZI NAKUMATT WALALAMIKIA KUKOSA MSHAHARA