Vituko mbalimbali hutokea katika mabunge ya nchi mbalimbali lakini March 21, 2018 kituko kingine kimetokea huko Jamhuri ya Kosovo ambapo katika Kikao cha Bunge la nchi hiyo, wabunge wa upinzani wameingia na gesi za machozi bungeni.
Wabunge hao waliwasha gesi hizo na kuvuruga mkutano huo ambao ulikuwa ukitaka kupiga kura kuhusu mpango wa ugawaji wa mipaka na Montenegro.
Inaelezwa kuwa walifungulia gesi hizo mara mbili kwa nyakati tofauti pindi kura hiyo ilipotakiwa kuanza kupigwa. Ilibidi polisi waingie bungeni humo na kuwatoa wabunge hao wa upinzani huku wabunge wawili wakiwa wamejeruhiwa.
BREAKING: Polisi kuhusu tukio la Afisa wa Syria kushambuliwa DSM