Kutokana na tuhuma ambazo zimeikumba kampuni ya Facebook hivi karibuni, akaunti za Facebook za kampuni za SpaceX na Tesla Inc zinazomilikiwa na Bilionea wa Afrika Kusini Elon Musk zimefutwa.
Elon Musk ameamua kufuta akaunti hizo ambazo zilikuwa na mamilioni ya followers baada ya kurushiana maneno kwenye mtandao wa Twitter na mtumiaji mwingine wa mtandao huo kuhusiana na akaunti za Facebook.
Musk alikuwa akimjibu Mwanzilishi Mwenza wa WhatsApp Brian Acton aliyekuwa amepost kwenye Twitter akiwaambia watu wafute akaunti zao za Facebook kwa kuuliza Facebook ni nini?
Baada ya Musk kuuliza hivyo, mtumiaji mwingine alimwandika na kumwambia afute akaunti zake zote za Facebook kama yeye (Musk) ni mwanaume kweli, jambo lililomfanya Musk kujibu kuwa atazifuta.
Mjadala huo umekuja baada ya Kampuni ya Facebook kutuhumiwa kuruhusu kampuni ya Cambridge Analytica kuchukua bila ruhusa taarifa za watumiaji wa Facebook ili kumpa ushindi Rais Donald Trump kwenye Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016.
Mama Ashura ndio sababu ya ukimya wa Ebitoke na Bwana Mjeshi? Wazungumza hapa