Leo March 24, 2018 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu Jenista Mhagama ameongoza zoezi la kuwakabidhi mikopo isiyokuwa na riba akina Mama 600 wa jiji la Arusha ikiwa ni marejesho ya fedha za madereva Pikipiki waliokopeshwa Pikipiki 200 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Mhagama amesema akina mama hao wanatakiwa kutumia fedha hizo katika makusudio ya kufanya biashara nakuahidi Ofisi yake kuendelea kutoa ushirikiano.
Nae Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema ameamua kuwakopesha akina mama kwa kuwa wamekuwa wakihitaji mtaji mdogo ili kutengeneza mazingira ya kufanya biashara zitakazowasaidia.
RC GAMBO AMEKABIDHI AKINA 600 MIKOPO AMEONGEA MKEWE KUUZA SUPU YA KONGORO