Polisi nchini Pakistan inawashikilia watu 12 wa familia mbili baada ya familia hizo kulipizana kisasi cha kubaka mabinti zao.
Inaelezwa kuwa binti wa moja ya familia hizo alibakwa na kijana wa familia nyingine, na hivyo suala hilo lilileta mtafaruku baina ya familia hizo mbili hadi kiasi cha kukaa kujadili muafaka.
Familia ya binti aliyebakwa waliambia familia hiyo nyingine kuwa sharti la kuwasamehe kutokana na kitendo hicho cha kijana wao kumbaka binti yao, ni kama kijana mmoja wa familia yao (ya binti aliyebakwa) pia atalipiza kisasi kwa kumbaka binti mmoja wa familia hiyo nyingine.
Polisi wanashikilia baadhi ya wanafamilia wa familia hizo mbili pamoja na viongozi wa kijiji hicho kwa jambo hilo.
BREKING: Kauli ya Uongozi UDSM kuhusu kusimamishwa Chuo kwa Abdul Nondo