Embu pata picha kama upo na familia yako au rafiki zako mmeenda kutembelea kwenye mbuga za wanyama halafu chui anaingia ndani ya gari lenu…! hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Britton Hayes na mjomba wake kutoka Seattle, Washington, walikuwa safarini kujionea wanyama katika mbuga ya taifa ya Serengeti nchini na chui akaingia kwenye gari lao, chui akawa mtalii ndani ya gari lao.
Mgeni huyo wasiyemtarajia alikaa ndani ya gari hilo kwa dakika 10 katika eneo la Gol Kopjes la mbuga hiyo, kabla ya mwishowe kuondoka kwenda kuwinda swala.
Britton Hayes anasema walikuwa wamemuangazia chui mmoja aliyekuwa ameruka sehemu ya mbele ya gari lao pale mwingine aliporuka na kuingia kupitia sehemu ya nyuma bila wao kumuona.
“Tulianza kugundua duma hao walikuwa wameanza kuvutiwa na gari letu, lakini hatukuwa na muda wa kuondoka au kutoroka kwa sababu hutaki kuwashtua wanyama hao, ukifanya hivyo ndivyo mambo huenda mrama,” Hayes aliambia jarida la Komo News.
BREAKING: “Silaha iliyomuua AKWILINA haijajulikana bado” -Kamanda Mambosasa
.