Stori ninayokusogezea leo March 31, 2018 ni kumhusu Muigizaji staa wa Hollywood Arnold Schwarzenegger amefanyiwa upasuaji wa moyo.
Arnold Schwarzenegger ambae amecheza katika filamu takriban 50 na alikuwa Gavana wa zamani wa California amefanyiwa upasuaji wa moyo ambao umemalizika salama.
Meneja wa nyota huyo amesema kuwa mnamo mwaka 1997 Arnold Schwarzenegger aliwekewa “pulmonary valve”,na upasuaji huu umefanywa ili kumuwekea “pulmonary valve” mpya.
Kama kawaida katika filamu zake Schwarzenegger hutumia sana neno la “I’ll be back”na baada ya upasuaji amerekodiwa akisema, “I am back”.
MAGAZETI LIVE: Askofu: ”2020″ chagueni Mtu sio Chama, Bombadier aliyofichua Lissu yaachiwa