Leo May 2, 2018 stori ya kuifahamu ni kumhusu Rais wa Marekani Donald Trump ambapo ameshuka nafasi 222 katika orodha ya kila mwaka ya watu matajiri zaidi duniani ambayo hutolewa na jarida la Forbes.
Mali yake imeshuka thamani kutoka $3.5 bilioni (£2.5bn) hadi $3.1 bilioni.
Jarida hilo limesema kushuka kwa utajiri wa Trump kumetokana zaidi na kushuka kwa thamani ya nyumba na vipande vya ardhi New York na pia kushuka kwa mapato kutoka kwenye viwanja vyake vya kuchezewa mchezo wa gofu.
Anayeongoza orodha ya matajiri wa kupindukia ni mmiliki wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos.
Utajiri wa Bezos umepanda na kufikia $112 bilioni kutoka takriban $39.2 bilioni mwaka jana. Kuimarika kwa utajiri wa Bezos ndiko kwa juu zaidi katika historia.
Amemuondoa mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates kutoka uongozini kwenye orodha hiyo.
Utajiri wa Gates unakadiriwa kuwa $90 bilioni mwaka huu kutoka $86 bilioni na ndiye anayeshikilia nafasi ya pili. Gates ameongoza orodha hiyo kwa miaka 18 kati ya miaka 24 iliyopita.
Forbes wanasema kuna mabilionea 2,208 (kwa kutumia dola za Marekani) ambao walishirikishwa katika orodha ya 32 ya kila mwaka ya jarida hilo.
Matajiri hao kwa pamoja wana utajiri wa $9.1 milioni.
Miongoni mwao, kuna mabilionea 259 wapya ambao walijipatia utajiri wao kutoka kutoakana biashara za aina nyingi zikiwemo nguo za harusi, wanasesere wa kuchezewa na watoto na magari yanayotumia umeme.
Mwekezaji mmarekani Warren Buffett ndiye wa tatu utajiri wake ukiwa $84bn. Utajiri wake umepanda kutoka $75.6bn mwaka uliotangulia.
MAGAZETI LIVE: Maumivu, Vyeti feki bado mtihani mzito, Kanisa lazuia shela maharusi wajawazito