Leo May 28, 2018 Kijana Dismas Benedicto mwenye miaka 27 mkazi wa Itahwa mkoani Kagera anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera kwa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu baada ya kuwadanganya wananchi kuwa shule ya Kembos imetangaza nafasi za kazi mbalimbali huku akiwataka watoe Rushwa ili wapate kazi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kagera, Augustine Ollomi amesema kijana huyo alikuwa ameshawatapeli watu zaidi ya 22 ikiwa ni sambamba na kutengeneza vitambulisho feki na stakabadhi mbalimbali za malipo.