Wakazi wa kijiji cha Kibiga wilayani Kiboga nchini Uganda wameachwa midomo wazi baada ya Waziri wa Jinsia Peace Mutuuzo akiwa ameambatana na wabunge 13 pamoja na baadhi ya maafisa wa wilaya hiyo kutoa msaada shilingi 45,000 za Uganda sawa na shilingi 27,281 za kitanzania kwa bibi kizee anayeishi na watoto yatima 10.
Fedha hizo ambazo alikabidhiwa bibi Teresa Namuli mwenye miaka 80 ziliambatana na kilo mbili za sukari pamoja na mikate wakati viongozi hao walipofanya ziara katika kijiji chicho.
Aidha mtu mmoja aliyetambulika kama Robert Katumwa alihoji inakuwaje wabunge hao pamoja na Waziri kutoa kiwango hicho kidogo cha fedha kwa familia hiyo wakati yeye sio Waziri lakini akiwa na fedha hujitolea kuwapa watu kiasi cha fedha kinachoanzia 10,0000 za kiganda ambazo ni sawa na 6000 za kitanzania au wakati mwingine hununua vitu na kuwapa watu”. .
Bibi huyo anayeishi kwenye nyumba dhoofu sana alimwambia Waziri kuwa kifaa chake kinachofua umeme wa jua kimeharibika na inahitajika shilingi 70,000 za kiganda kukirekebisha na Waziri alimjibu kuwa atalishughulikia suala hilo mara tu atakapofika Kampala.