Mbunge mmoja wa nchini Urusi amewapa ushauri Wanawake wa Urusi kuwa wasijiingize katika mahusiano na Wageni waliokwenda nchini humo kutazama Kombe la Dunia kwa kile alichokidai watawaumiza kimapenzi.
Tamara Plentyova ambaye ni mkuu wa kamati ya familia, Wanawake na masuala ya Watoto bungeni amesema kuwa Wanawake wa Urusi wasijiingize kwenye mahusiano na Wageni kwani wataishia kuumizwa hata kama wakipata watoto bado baba zao wataondoka nao kitu ambacho kitazidi kuwaumiza.
“Mkijiingiza kwenye mahusiano na wageni baadaye mtakuja kwangu mkilia kwamba watoto wenu wamechukuliwa” amesema Tamara.
Aidha Tamara aliongeza kuwa Wanawake waliopata watoto na raia wa kigeni wakati wa michezo ya Olimpiki ya 1980 mjini Moscow walisalia kuwa wanawake wasio na Wanaume.
LIVE MAGAZETI: Watapigwa kipigo cha Mbwa koko!, Bajeti yang’ata yapuliza