Leo July 3, 2018 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi kwa baadhi ya mikoa.
Katika mabadiliko hayo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Deusdedit Nsimeki aliyekuwa Makao Makuu ya upelelezi Dar anakwenda kuwa RPC wa Simiyu.
RPC wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Ulrich Matei anakwenda kuwa RPC wa Mbeya na Kaimu RPC wa Mbeya Kamishna Msaidizi, Mussa Taibu amehamishiwa Makao Makuu Dar.
RPC wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Wilbroad Mutafungwa anakuwa RPC wa Morogoro, nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi, Emmanuel Nley kutoka Makao Makuu Dar.
Katika Mabadiliko mengine, Ofisa Mnadhimu wa Geita Kamishna Msaidizi, Stanley Kulyamo anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Tazara.
IGP Sirro amewataka Makamanda wa Polisi wa mikoa nchini, kuendelea kuwajibika ipasavyo katika kuhakikisha ajali hazitokei katika maeneo yao.
Afande Sele “JPM ukicheka na nyani utavuna mabua”