Leo July 24, 2018 Rais wa Marekani, Donald Trump na Rais wa Iran, Hassan Rouhani wamejibizana vikali na kutoleana vitisho huku uhasama baina ya mataifa hayo mawili ukiongezeka.
Trump ameandika katika Twitter yake, kwa herufi kubwa, kwamba “Iran itapata madhara ambayo ni wachache sana wamewahi kukumbana nayo katika historia iwapo itaitishia Marekani.”
Kwa upande wake Rais Rouhani awali alikuwa amesema kwamba sera za uadui za Marekani dhidi ya Iran zitasababisha vita ambavyo vitakuwa “vita zaidi ya vita vingine vyote.”
Ikumbukwe kuwa May mwaka huu, Marekani ilijitoa kwenye mkataba wa nyuklia na Iran ambao ulikuwa umehusisha Iran kusitisha shughuli zake za nyuklia ili iondolewe vikwazo vya kimataifa.
Marekani sasa imeanza kuiwekea tena Iran vikwazo licha ya pingamizi kutoka kwa Uingereza, Ufaransa, China, Urusi na Ujerumani wote ambao walikuwa wadau katika mkataba huo wa mwaka 2015.
MAGAZETI LIVE: Watu 65 wajiua Geita, Watu wa 5 kunyongwa hadi kufa, JPM afichua mbinu