Leo July 24, 2018 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ameivunja Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Akitangaza uamuzi huo Jijini Dodoma Waziri Mhagama pia ametengua uteuzi wa wajumbe wote wa bodi hiyo na utaratibu wa uteuzi wa bodi mpya unafanyika
Waziri ametaja baadhi ya maeneo ya kiutendaji yanayohitaji kuimarishwa ni pamoja na kuongeza wanachama, kukusanya michango, kulipa mafao kwa wakati na kusimamia vitega uchumi vya shirika kizalendo.
“Wewe nishakuonya unasema RC Mwanza hapajui mjini ana njaa” Mongella