Leo August 6,2018 tunayo story kutokea kijiji cha Chamakweza kilichopo Kata ya Vigwaza mkoani Pwani ambapo kinaelezwa hakina Zahanati tangu mwaka 1975.
Akizungumza kwenye mkutano wa Diwani wa Kata ya Vigwaza, Mohsin Bharwani na Wanakijiji, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Mika Kashima amesema miongoni mwa changamoto zinazokikabili kijiji hapo ni ukosefu wa Maji na Zahanati.
Kashima amesema huduma za kiafya zimekuwa tatizo kijiji hapo na wanalazimika kuitafuta kwa umbali mrefu.
“Hatuna zahanati tangu mwaka 1975, wajawazito wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za kiafya, hivyo tunamuomba Diwani atusaidie katika hili,” amesema Kashima.
Kutii agizo la JPM mabingwa wa uzalishaji Viazi wakutanishwa Mbeya