Mfanyabiashara raia wa China anaeishi nchini Kenya, Liu Jiaqi amekamatwa kufuatia kusambaa kwa video yake katika mitandao ya kijamii inayomuonesha akiwakashifu raia pamoja na Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta.
Taarifa ya uhamiaji nchini Kenya imesema “Kibali chake cha kazi kimefutwa na atafukuzwa nchini kutokana na ubaguzi”.
Video hiyo iliyosambaa katika katika mitandao ya kijamii inamuonesha mfanyabiashara huyo akirekodiwa na mfanyakazi wake huku akisema, “Kila mmoja, kila mkenya ni kama nyani, akiwamo Uhuru Kenyatta, hao wote”.
Aliposhauriwa na mfanyakazi huyo kuwa arejee kwao China endapo hapendi kuendelea kuishi Kenya, alijibu, “Mimi si mkazi wa hapa, sipapendi hapa, watu wake ni kama nyani na sipendi kuongea nao, pananuka harufu mbaya, masikini na watu ni weusi, siwapendi. Kwanini hawako kama watu weupe, kama wamarekani ?”.
Kwa mujibu wa msemaji wa ubalozi wa China nchini Kenya, Zhang Gang, video hiyo ilirekodiwa mwezi Juni na tayari alishachukuliwa hatua na kampuni yake kwa kitendo hicho huku akiwaomba radhi wakenya kwa tukio hilo.
Mpishi alivyoweka Bondi nyumba kisa Hotel (+video)