Club ya Man United katika mechi zake za hivi karibuni za mwanzo wa msimu zimeanza kwa wao kutokupata matokeo chanya katika baadhi ya mechi, kiasi cha kuanza kuleta tetesi kuwa kocha wao Jose Mourinho anaweza akafutwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na Zidane.
Man United kwa sasa wanajiandaa na mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Valencia hivyo kocha wao Mourinho, ameamua kuweka wazi mpira jinsi ulivyo baadhi ya wachambuzi wanapaswa kumuheshimu na kuanza kumjaji akiwa msimu wa tatu Man United.
“Kabla ya yote katika mpira kama unataka kuujua kisayansi, kama unataka kuchambua ni namna gani mchezo ulivyo na namna gani unaweza kuwa, Real Madrid alipoteza 3-0, Barcelona ndani ya game mbili amepoteza point tano, AC Milan katoka sare na Empoli timu ambayo ndio kwanza imepanda daraja huo ndio mpira”
“Lakini unajua kuna wakati najihisi kuchanganyikiwa kwa sababu kazi tunayoifanya na ninachokitoa katika mchakato, siku zote nakuwa natarajia makubwa, tumejifua vizuri sana hivyo kesho na tarajia mchezo mzuri”
“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga