Kuna baadhi ya ujuzi wengi wetu tumezoea kuona mtu akipata akiwa katika vyuo ambavyo vinatoa Taaluma hiyo baada ya kumaliza aidha kidato cha Nne au form six nakujiunga na chuo.
Fani ya udaktari wa binadamu watu wengi ujua wakiwa wamefika Chuo na kupata taaluma hiyo lakini kwa Mwanafunzi Eda Bwakisa na wenzake wa Darasa la Sita katika shule ya Msingi ya Feza iliyopo jijini SM ni tofauti sana kwani kwasasa wameshafundishwa na kujua jinsi ya kupima mtu yupo katika kundi gani la damu kama wataalamu wa maabara wanavyofanya.
Mwalimu Benard Odenyi anaye wafundisha wanafunzi hao amesema imewachukua miezi miwili wanafunzi hao kuelewa kivitendo ukiachilia muda wa darasani ambao pia hufundishwa masomo hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule za Fedha, Ibrahim Yunus anasema elimu si darasani tu ndio mana wanaonyesha majaribio hayo ili kutambua uwezo wa yale waliyofundishwa darasani kwa kuonyesha kwa vitendo kwa yale ambayo anatakiwa kuonyesha kwa jamii.
Naye Mhadhiri wa Chuo kikuu cha DSM kutoka idara ya Kemia Daktari Clarance Mgina amesema wanasayansi wanapoanzishiwa tangu shule ya msingi inasaidia kupata wanansaynsi wazuri tangu utotoni.
Mtoto jasiri Anthony anafundisha wenzie Kiingereza, akumbushia shamba lao