Chama cha soka England FA kimetangaza kumuadhibu kocha msaidizi wa club ya Chelsea Marco Ianni kwa kitendo chake cha kushangilia goli la Chelsea mbele ya benchi la ufundi la Man United wakati wa timu hizo zililipokutana.
FA imefikia maamuzi ya kumpiga faini Marco Ianni ya pound 6000 ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 22 kutokana na kitendo hicho cha kushangilia goli la Chelsea la kusawazisha mbele ya Jose Mourinho.
Chelsea na Man United walikutana October 20 2018 katika uwanja wa Stamford Bridge ambapo Chelsea walisawazisha goli dakika za nyongeza kupitia kwa Barkley na kufanya matokeo 2-2, kitu ambacho kilimfanya Ianni ashangilie mbele ya Mourinho na kutafsiriwa kama kafanya kejeli.
Da!!! Takwimu za Samatta Ligi Kuu Ubelgiji msimu huu ni hatari