Mtanzania aliyeunda BAJAJI, Mzee Andrew Mbanga ambapo amesema ni miezi miwili imepita tangu BAJAJI yake ipelekwe Chuo cha Taifa cha Usafarishaji (N.I.T) kwa ajili ya kurekebishwa kutokana na agizo alilolitoa aliyekuwa Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage.
Mzee Mbanga amesema hadi Mwijage anatenguliwa kwenye nafasi yake ya Uwaziri na Rais John Magufuli bado BAJAJI hiyo haijarekebishwa kama alivyotoa maagizo pamoja na fedha kwa ajili ya kuirekebisha.
“Hadi leo hakuna mrejesho waziri alishatoa nguvu zake, BAJAJI iliagizwa ikatwe hadi sasa haijakatwa kwani Mainjinia walifatilia makosa madogo madogo ambayo yametakiwa yarekebishwe japo tatizo kubwa ilikuwa ikatwe lakini nikiuliza wanasema iongezwe pesa ifike Laki Tano na arobaini kwa ajili ya vifaa,”amesema.
Mzee Mbanga amesema anapa athari kubwa kwa kuwa akili yake imejikita kutengeneza BAJAJI, hivyo kukwama huko kunamkatisha tamaa kwani anatarajia kufungua kiwanda.
SAKATA LA USHOGA: MUFTI MKUU TANZANIA ATOA KAULI ‘MUNGU ALIANGAMIZA KIJIJI’