Club ya Yanga SC leo imethibtisha rasmi kumsajili kiungo mahiri wa African Lyon Haruna Moshi Boban kwa ajili ya kukikongezea nguvu kikosi chao kwa ajili ya mikiki mikiki ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika ameripotiwa kukamilisha usajili wa mchezaji huyo na sasa anatuwa rasmi Jangwani, baada ya usajili huo kocha mkuu wa Yanga raia wa Congo na Ufaransa Mwinyi Zahera ameeleza namna alivyovutiwa na Boban.
“Nilikuwa katika ofisi ya Ndama sasa nikaona katika TV kuna mechi ya African Lyon na JKT, ndio nikamuona Boban katika TV ndani ya ofisi ya Ndama, namuona mchezaji mmoja alipiga pasi ambayo imenivutia nikamwambia Ndama muone huyu mchezaji ananikumbusha mchezaji mmoja hivi”>>>Mwinyi Zahera
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Haruna Moshi Boban amewahi kucheza soka katika vilabu mbalimbali nchini Tanzania kama Moro United, Simba SC, Mbeya City na soka la kulipwa katika klabu ya Gifle IF ya Sweded, hivyo anaingia Simba baada ya kuonesha uwezo mkubwa tena.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe