Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 imeendelea tena leo kwa michezo kadhaa kuchezwa ila game iliyokuwa inafuatiliwa sana ni game kati ya Singida United dhidi ya Yanga katika uwanja wa Namfua, uwanja ambao ulikuwa ukilalamikiwa kuwa haupo sawa na game itakuwa ngumu.
Game hiyo ilikuwa ngumu kama ilivyotazamiwa kwani dakika 90 zilimalizika kwa timu kutoka sare tasa 0-0, huku baadhi ya wachambuzi wakiamini kuwa ubovu wa uwanja umesababisha timu hizo kushindwa kucheza soka safi, Yanga wanaendelea kupoteza point zaida.
Baada ya sare ya leo Yanga anakuwa kapoteza point 4 mfululizo kutokana na kutoka sare ila anaendelea kuongoza Ligi kama kawaida kwa kuwa na pont 55, ila anajiweka katika nafasi ya hatari zaidi kushwa kileleni kama wapinzani wao Simba wakiweza kushinda game zao zote za viporo.
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF