Mahakama ya Rufani Tanzania imetupilia mbali rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko kuhusu kupinga dhamana.
Pia mahakama hiyo imeagiza jalada la kesi hiyo lirudishwe Mahakama Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa rufani iliyokatwa na Mbowe na Matiko kupinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana zao.