Kamati ya Malalamiko imeundwa kutokana na kifungu cha 20 (1) cha sheria iliyounda Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003 ambacho kinatoa fursa ya kuundwa kwa kamati ndani ya
Mamlaka kusimamia masuala mbalimbali.
Baada ya kupokea malalamiko Kamati itaita pande zote na kuzisikiliza na itatoa uamuzi ndani ya siku 30 hadi 60. Upande ambao hauridhiki na uamuzi wa Kamati unaweza kukata rufaa kwenye Baraza la Uamuzi wa Haki (Fair Competition Tribunal–FCT).
Utaratibu unataka Mamlaka ijulishwe juu ya uamuzi wa kukata rufaa. Malalamiko yanayohusiana na maudhui ya utangazaji yatasikilizwa na Kamati ya Maudhui.