Mahakama Kuu ya Tanzania imetengua hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo ilimuhukumu Bob Chacha Wangwe kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela au kulipa faini ya Shilingi Milioni 5 baada ya kupatikana na hatia kwenye kosa la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa Facebook.
Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Kuu kutokana na rufaa iliyokatwa na Wangwe baada ya kuhukumiwa na Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kusema katika kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 6 na vielelezo 5 dhidi ya Bob ambae pia ni Mwanaharakati.
Miongoni mwa sababu zilizotolewa na Mahakama Kuu ni kwamba Wangwe alitiwa hatiani kimakosa na baadhi ya mashahidi muhimu wakiwemo TCRA hawakupelekwa mahakamani hivyo adhabu aliyopewa imefutwa.