Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jenerali Emanuel Maganga amesema kuwa Serikali Mkoani humo itahakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika kwa kuongeza Vikosi vya Usalama katika maeneo ambayo yamekumbwa na vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na majambazi wanaotumia silaha za moto.
RC Maganga ametoa kauli hiyo wakati wa mazishi ya Bi. Sophia Thomas aliyefariki baada ya kujeruhiwa kwa risasi na majambazi waliovamia katika Mji wa Kibondo March 30 mwaka huu.