Baada ya maswali kuwa mengi na subiri kuwepo kwa muda mrefu muwekezaji wa club ya Simba SC Mohammed Dewji MO leo amekutana na waandishi wa habari na kuongea nao mambo mbalimbali kuhusiana na club hiyo hususani uwanja wa Bunju ambao ulikuwa unatazamiwa uanze kutumika mapema mwaka huu.
MO amethibitisha nyasi bandia za Simba zilizokuwa zinashikiliwa bandarini tayari wameshamalizana na mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa TAKUKURU kuhusiana na kuhusu uwanja huo wanategemea kuanza kuufanyia mazoezi mwezi May 2019.
Ukimuuliza Mwinyi Zahera ishu za Ajib kurudi Simba SC….