Kama unamkumbuka Oscar Pistoriuos mwanariadha wa South Africa ambae alimiliki vichwa vya habari kutokana na kumuua kwa risasi girlfriend wake siku ya wapendanao Feb 14 2013, kesi yake inaendelea Mahakamani kuhusu hayo mauaji.
Sasa amelazimika kuuza nyumba yake ili kulipia gharama zinazotokana na mkasa wake mkubwa wa kisheria kwenye hii kesi ya kumuua Reeva Steenkamp.
Mwanariadha huyo amekubali kumpiga risasi mwanamke huyo aliefariki akiwa na umri wa miaka 29 lakini amekataa tuhuma za mauaji hayo akisisitiza alikosea na kudhani amevamiwa nyumbani kwake.
Pistorious ambae ni mlemavu wa miguu miwili akiwa na umri wa miaka 27 sasa hivi,a nawakilishwa na timu inayoongozwa na mwanasheria mashuhuri Barry Roux.
Iliripotiwa mwaka jana kwamba Pistorious alilazimishwa kuuza mali zake kadhaa baada ya kuwa na bili za kisheria za kiasi cha £200,000 ambapi pia alilazimika kulipa kiasi cha sh £73,000 baada ya kupewa nafasi ya kupata dhamana.
Mikataba ya udhamini wake kutoka kwa Kampuni za Nike na Oakley imeisha hivyo Pistorious ameomba marafiki kumsaidia aweze kuuza mali zake ili kukuza pesa kwa ajili ya kesi hiyo.
March 20 2014 mwanasheria wake amethibitisha kuwa Pistorious ameuza nyumba yake Pretoria ambayo ndiko alikofia Reeva na kusema ni muhimu kumaliza gharama zaidi za kesi hiyo ambazo zinaendelea kupanda kwa sababu pia Pistorius hatoweza kurudi kuishi pale tena.
“Ameiuza hii nyumba pia kutokana na kuongezeka kwa muda wa hukumu bila mategemeo ambapo ni zaidi ya wiki tatu tofauti na ilivyopangwa mwanzoni”
Hii nyumba ilikua imefungwa tangu irudishwe kwa Pistorius kutoka kwa polisi mwaka 2013 ambapo kesi hii ya mauaji imekutana na mfululizo wa ucheleweshaji kutokana na upepelezi uliokuwa ukiendelea na kuna uwezekano itaendelea kukaa zaidi kortini baada ya mashtaka haya kutangaziwa kuwa na orodha ya mashahidi zaidi ya 100.
Mshtaka mkuu Gerrie Nel alisema atakua akiita wanne au watano ili kesi imalizike mapema ambapo pia Pistorius anaweza kuendelea kutoa ushahidi mapema wiki ijayo.