Timu ya taifa ya Misri ambayo ni Mabingwa wa AFCON mara saba wametoa dalili nzuri katika michuano hiyo baada ya ushindi dhidi ya Congo DR katika mchezo wa Kundi A, Misri wamefikisha point sita katika Kundi lake na kuleta matumaini.
Misri wamefikisha point sita huku wakivunja mwiko wao wa kucheza game za AFCON na kutoshinda magoli zaidi ya 2 na kuendelea toka 2010 walipoifunga Algeria 4-0, wakati kufunga goli kwa MO Salah la pili katika ushindi wa Misri dhidi Congo wa 2-0, linamfanya aweke rekodi ya kufunga magoli 40 timu ya taifa na kuwa mfungaji wa tatu wa muda wote wa Misri.
VIDEO: Inabidi Muielewe tu Taifa Stars, Msuva Kaongea Kwa Hisia