Winga wa Taifa Stars Simon Msuva ambaye alikuwa mfungaji wa goli la kwanza la dakika ya 5 la Taifa Stars katika mchezo dhidi ya Kenya licha ya kupoteza 3-2, ameongea na waandishi wa habari na kueleza hisia zake kuwa wameumizwa na matokeo hayo kama wachezaji na haikuwa lengo lao.
“Huo ndio mpira ambao una matokeo matatu kuna kushinda, kufungwa na sare sisi tumepoteza huu mchezo tulitamani kushinda lakini wenzetu wameshinda kwa upande mwingine tumeumia kama wachezaji na watanzania najua wameumia”>>> Simon Msuva
Timu ya taifa ya Tanzania mchezo wao wa mwisho watacheza July 1 2019 dhidi ya timu ya taifa ya Algeria walio vinara wa Kundi C kwa kuwa na jumla ya point 6, Senegal wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na point tatu tofauti ya magoli dhidi ya Kenya waliopo nafasi ya tatu wakati Tanzania ikiburuza mkia.
“Mimi naamini kuanguka ni kujifunza bado tupo kwenye mashindano”-Samatta