Mbwa mashuhuri kwa kunusa, Frida, ambaye aligonga vichwa vya habari wakati wa mkasa wa tetemeko la ardhi lilioua watu zaidi ya 350 katika Mji wa Mexico mwaka wa 2017, hatimaye amestaafu.
Frida amestaafu baada ya kuhudumu na jeshi la wanamaji la Mexico (Semar) kwa zaidi ya miaka 10. Sherehe ya kustaafu kwake ilifanyika Ijumaa iliyopita katika makao makuu ya Semar, mjini Mexico.
Frida ameshiriki operesheni za uokoaji nchini Ecuador, Haiti na Guatemala, katika kipindi hicho cha miaka 10, Farida ametambuliwa kwa kuokoa manusura 12 wa majanga ya asili.