July 4, 2019 Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amezungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake na kuelezea hali ya usalama ilivyo katika mkoa wake ambapo pia ametolea maelezo ya baadhi ya matukio ya uhalifu yanayoendelea huku miongoni mwa hayo ikiwa ni tukio la kijana wa kiume aliyeuawa na Wananchi kufuatia kufanya tukio la kuwabaka watu watatu akiwemo kikongwe kwa nyakati tofauti.
“Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30 majina yake hayajafahamika alibaka watu watatu kwa nyakati tofauti, tukio la kwanza alimbaka bibi kizee aliyemvizia chooni kisha kumkaba na kumbaka, tukio la pili alimbaka mtoto wa miaka minne baada ya kumvutia kichakani na kumbaka”-Gilles Muroto
“Tukio la tatu alimbaka mtoto wa miaka minane mwanafunzi wa darasa la pili baada ya kumkamata kwa nguvu kwenye pagala la nyumba ambapo wananchi walimkamata na kumshambulia kwa kipigo”-Gilles Muroto