Polisi Temeke imethibitisha kumshikilia Khamisi Luongo kwa kosa la kumuua mke wake Naomi Marijani aliyedaiwa kupotea kwa zaidi ya miezi miwili na picha yake kusambazwa mitandaoni,Luongo amekiri kumuua mkewe kisha kumchoma kwa mkaa magunia mawili na kuyazika majivu shambani kwake.
“Baada ya kumuua mke wake na kuuteketeza mwili kwa moto, Luongo alichukua majivu akaweka kwenye mfuko na kubeba kwa kutumia gari lake lenye namba T206 CEJ, Subaru Forester yenye rangi nyeusi na kuyapeleka shambani kwake katika Kijiji cha Mlogolo, Mkoani Pwani”-Polisi Temek
“Mtuhumiwa (Luongo) tunamshikilia, katika maelezo yake amedai baada ya kumuua mke wake aliuweka mwili kwenye shimo alilochimba katika banda la kufugia kuku. akaweka mkaa magunia mawili na mafuta ya taa kisha akawasha moto ulioteketeza mwili wote hadi kubaki majivu”- Polisi Temeke