Leo September 21, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa ameitisha mkutano wa Wananchi wote wa Wilaya ili wasikilizwe kero zao kwa pamoja na kupata ufumbuzi.
DC Kissa Taasisi zote ambazo zipo ndani ya Wilaya yake na nje huku akiwa kaita Mawakili zaidi ya 40 ambao kazi yao itakua ni kutoa ushauri wa kisheria kuhusu migogoro ya Ardhi, ndoa na mirathi na mambo mengine.
“Nakemea leo tabia ya Watumishi wa Serikali kutosikiliza na kuwahudumia Wananchi vizuri wanapokuja Ofisini, hawa ndi Maboss wetu sisi Serikali, kama mimi Mkuu wa Wilaya natoa kiti ofisini nakaa parking, iweje wewe Mkuu wa Idara, iweje wewe mtumishi” DC Kissa
Hayo yametokea baada ya Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Mzava kulalamikia kero ya migogoro ya ardhi na Vitambulisho vya Taifa pamoja na vya kuzaliwa ambao anakumbana nazo kila akiongea na wananchi.