NI Msiba kutokea nchini Kenya ambapo mwisho wa wiki iliyopita waliripoti habari kuzama kwa gari lililokuwa na watu wawili Miriam Kiganda na Amanda Muzehu (Mama na mwanae) huko feri ya Likoni Mombasa.
Shirika la feri nchini humo kupitia mkurugenzi wake Bakari Gowa akizungumza na waandishi wa habari leo alisema amesitisha shughuli za uchukuzi wa kivuko hicho cha Likoni ili shughuli za kutafuta miili iendelee.
Wanaoendesha shughuli hiyo ya upoaji kwasasa wanalenga maeneo mawili ili kulifikia gari hilo ambalo limekwama kwenye sakafu ya bahari.
Kufikia saa kumi na moja leo jioni October 1, 2019 shughuli hiyo ilikuwa imesitishwa tena kutokana na ukosefu wa vifaa vinavyowezesha kuona chini ya bahari nyakati za usiku.
Familia ya Marehemu kwa upande wao wanaimani miili ya wapendwa wao itapatikana kwani wanasema wameanza kuwatumia wapoaji binafsi ili kusaidia kutafuta miili ya wapendwa yao.
Unaweza ukaitazama hii video hapa ujione namna kituo cha TV Citizen nchini Kenya wanavyoripoti kuhusiana na tukio hilo la kuzama kwa gari hilo
UJIONEE MKURUGENZI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KUSITISHWA KWA HUDUMA A FERI KATIKA KIVUKO CHA LIKONI