Wanafunzi wa Kidato cha Tano na cha Sita zaidi ya 150 katika Shule ya Sekondari ya Kiwanja Wilayani Chunya Mkoani Mbeya wameunguliwa na vitu vyao usiku wa kuamkia October 1, 2019 kufuatia mabweni mawili kuteketea kwa moto huku chanzo cha moto huo kikiwa bado kinachunguzwa.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chunya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Maryprisca Mahundi ilifika haraka eneo la tukio na kuweka ulinzi madhubuti kuhakikisha moto hauteketezi mabweni mengine.
“Nimesikitishwa sana na tukio hili hasa ikizingatiwa serikali inafanya kila namna kuboresha miundombinu ya elimu nchini ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi na shule ya Kiwanja licha ya kuwepo Chunya lakini inapokea wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali nchini” DC Mahundi
MKUU WA MKOA ALIVYOWACHARAZA VIBOKO WANAFUNZI 13 HADHARANI
https://youtu.be/y3fvQmKq744