Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Erick Mapunda kuyavunja Mabaraza yote ya Kata na Vijiji ya ardhi yasiyotenda haki wakati wa kutoa maamuzi katika wilaya ya Mafia mkoani Pwani.
Alisema, kutokana na kero nyingi za ardhi alizozipokea katika ziara yake hiyo wilayani Mafia amebaini Mabaraza ya Kata na Vijiji katika wilaya hiyo hayafanyi kazi zake vizuri na wajumbe wake wamekuwa wakiyatumia kutoa maamuzi yasiyozingatia haki.
Baadhi ya wananchi wa Mafia wamelalamikia Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji katika wilaya ya Mafia pamoja na kero nyingine mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa zinachangia uwepo migogoro ya ardhi.
Mohamed Shaban na Aisha Mohamed ni miongoni mwa wananchi wa Mafia waliowasilisha kero zao kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na hapa wanazungumza.
MKUU WA MKOA ALIVYOWACHARAZA VIBOKO WANAFUNZI 13 HADHARANI
https://youtu.be/y3fvQmKq744