Mkuu wa Mkoa Mbeya, Albert Chalamila amewaondoa Shuleni wanafunzi wote wa Kidato cha Tano na Sita ktk Shule ya Sekondari Kiwanja na kuwaamuru warudi nyumbani hadi October 18, 2019 na watakaporejea kila mmoja awe amelipa Shilingi 200,000 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni yaliyochomwa moto.
“Mtakumbuka jana nilikuwepo hapa nilipiga vijana viboko, wengine wamenijadili sana kwenye mitandao kwamba Mkuu wa Mkoa anatoa wapi Mamlaka haya, Mkuu wa Shule Boss wake ni Mkuu wa Mkoa kama yeye anaruhusiwa kuwachapa basi mimi natakiwa niwacharaze sana”-RC MBEYA
MKUU WA MKOA ALIVYOWACHARAZA VIBOKO WANAFUNZI 13 HADHARANI
https://youtu.be/y3fvQmKq744