Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amepokea taarifa ya ujenzi wa barabara aliyoikagua na kukuta ina mpasuko ambapo kupitia taarifa hiyo Mamlaka ya Usimamizi wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA Mkoa wa Tabora imekiri kuwepo kwa kasoro zilizofanywa na Mkandarasi CICO anayejenga barabara hiyo yenye zaidi ya Kilomita tano.
Akipokea taarifa hiyo Mwanri ametaka kuwepo kwa usimamizi madhubuti katika miradi hiyo “katika mradi huu mshauri amechukua Milioni 400, sasa Milioni 400 zinachukuliwa halafu inapiga cleck nataka habari hiyo mnaimaliza huko huko kwenye site” RC MWANRI