Mara nyingi imezoelekea kwa vyombo vya habari mbalimbali vya habari Duaniani kama BBC ya UK, VOA ya America na DW ya Ujerumani kufungua radio au vipindi vya TV vitavyotoa maudhui kwa lugha ya Kiswahili lakini sio kwa club ya Ulaya kutoa habari zake kupitia page rasmi za mitandao ya kijamii kwa lugha ya Kiswahili.
Club ya AS Roma ya Italia leo inaandika historia ya kuwa club kubwa ya kwanza Ulaya kuwa na ukurasa rasmi wa twitter wa kutoa/kuandika habari zake kwa Kiswahili, AS Roma wana page za Lugha zaidi ya 8 zikiwemo (Kireno, English, Pidgin, Espanyol, Kiarabu, Persian, Bosnia na Femminile).
AS Roma jumapili walitangaza kuwa Jumatano watazindua rasmi ukurasa wao wa twitter wa habari za Kiswahili, haijawahi kutokea katika soka club za soka Ulaya kuanzisha ukurasa rasmi wa kutoa habari zake kwa lugha ya Kiswahili ila zimekuwa na kurasa rasmi za lugha kama za kiingereza, kifaransa, kihispaniola lakini Kiswahili ndio kwa mara ya kwanza.
AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI