Baada ya kufanywa kwa utafiti na uchunguzi wa kina kuhusiana kukosekana kwa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wanaohitimu mafunzo ya Tehama, Ruse Telecom kupitia kwa CEO wao Halima Idd wametangaza kutoa mafunzo hayo kwa vitendo kuboresha ufanisi kwa wanafunzi.
“Changamoto kubwa tunayokumbana nayo tasnia ya TEHAMA (ICT) upungufu wa ujuzi kwa vitendo, mfano Mwanafunzi amemaliza mtihani anarudi mtaani inakuwa ni ngumu sana kwake kupata ajira kwa sababu hana ujuzi wa vitendo na kama tunavyojua waajiri wengi sana tayari ana ujuzi hana muda wa kuanza kumfundisha yeye yupo kwa ajili ya biashara”>>> Halima Idd
“Juzi juzi tulikuwa zama za 2G sasa hivi tupo 4G na sasa tutaingia 5G hauwezi kujua sasa hivi tunaongelea vitu data sasa hivi ndio mambo ya Cloud tunaongelea artificial tunaongelea Cyber Security vitu kama hivi havifundishwi shuleni”>>>Halima Idd
“Kwa hiyo wale wanafunzi wanakuja wanakaa mtaani hawawezi kujiari wala kuajiriwa mwisho wa siku wanakaa tu, Ruse imeona hiyo changamoto ndio maana imefungua hii platform kuhakikisha kwamba tunatoa mafunzo ya muda mfupi kuanzia wiki moja hadi miezi mitatu hapa Tanzanite Park Victoria”>>>Halima Idd
VIDEO:CEO WA SIMBA , ALIPOULIZWA HATMA YA AUSSEMS KWAKUTOFIKIA TARGET