Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amempa siku mbili Afisa Madini Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho kupeleka ofisini kwake taarifa kuhusu mgogoro uliodumu kwa kipindi kirefu wa mgodi wa Magambas uliopo wilayani Handeni Mkoani Tanga unaondelea kuikosesha Serikali mapato kwa muda mrefu sasa.
‘‘Nikutake Afisa Madini mkoa kupeleka taarifa siku ya jumatano mezani kwangu inayoelezea kwa kina kuhusu mgodi huo na endapo nikigundua kina mambo ya kizembe yanaendelea basis sitosita kumuwajibisha anayehusika hatuwezi kuikosesha serikali mapato kwa uzembe,”alisisitiza Naibu waziri Nyongo.
SUMAYE, MBOWE WATAJWA UENYEKITI CHADEMA TAIFA, TUNDU LISSU AACHIWA NA KUBENEA