Wakati Dunia na Serikali ya Tanzania ikipambana juu ya matukio ya ubakaji, Ayo Tv na Millardayo.com imezungumza na familia ambayo Baba amebaka watoto wake wanne wakiwemo wakiume.
AyoTV imefunga safari ya takribani Kilomita 50 kutokea jijini Dar es Salaam hadi kufika Kijiji cha Homboza, Kisarawe mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuzungumza na familia hiyo.
“Siwezi kumsamehe Baba, nipo tayari kuwa shahidi mahakamani, wakati ananibaka alikuwa akiniingiza vidole mdomoni ili nisitoe sauti,” Mtoto wa miaka 13
“Alinambia wazazi wote wakiume wanawafanyia hivi watoto wao wakike ili wawe wasichana wazuri,”.
Hadi sasa tayari Jeshi la Polisi linamshikilia Baba huyo na anatarajia kufikishwa mahakamani.
Katika ripoti iliyotolewa Mei 15, 2019 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustin Ndugulile akiwa Bungeni mjini Dodoma alisema ongezeko la matukio ya ubakaji katika kipindi cha Desemba 2015 yalikuwa 394 na yakaongezeka hadi kufikia 2,984 kwa Desemba 2017 ambalo ni ongezeko la matukio 2,590.
MTOTO MWENYE UWEZO MKUBWA WA KUTAJA MAJINA YA VIONGOZI, AANZA SHULE KWA MARA YA KWANZA