Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewasili makao makuu ya ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa asubuhi ya leo, Januari 31.
Lugola anatuhumiwa kusaini ununuzi wa vifaa vya zimamoto na uokoaji vyenye thamani ya Tsh trilioni 1.04 kutoka kampuni ya nje ya nchi bila kufuata sheria.
Januari 23 Rais Dkt Magufuli alisema kuwa katika mchakato wa zabuni ya ununuzi wa vifaa hivyo baadhi ya viongozi wa jeshi la zimamoto na uokoaji walikuwa wakikaa kwenye vikao na kulipwa posho Tsh milioni 1.8, ambapo Tsh milioni 1.2 ilikuwa ni posho ya kikao na Tsh laki 6.9 ikiwa ni posho ya safari na tarakilishi mpakato (laptop) kwa kila mmoja kila walipokutana.