Rais Dk. John Magufuli amemfukuza kazi mtumishi wa umma aliyechana kitabu cha Quran Tukufu mkoani Morogoro na amemuagiza Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleimani Jafo amuandikie barua ya kumfukuza.
“Juzi nilikuwa namsikiliza Waziri Jafo yupo Mtumishi alichana Quran nafurahi umemsimamisha kazi, lakini naagiza afukuzwe moja kwa moja, ashinde keshi asishinde ila aondoke, muandikie barua ya kumfukuza, akitoka huko atajua mwenyewe atakakoyatafuta Maisha”– JPM