Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isack Kamwelwe amesema ujenzi wa daraja Kiegeya unatarajiwa kumalizika leo usiku na ifikapo majira ya saa 3:30 usiku magari yataanza kupita.
Daraja hilo lililopo Wilayani Gairo, katikati ya maeneo ya Magubike na Kiegeya lilibomoka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mawasiliano ya barabara ya Morogoro-Dodoma kukatika.